Diamond na Ney wa Mitego |
Godzilla |
Mabeste |
Madee |
Prod. wa Mj Records ,Marco Chali akitoa maelezo kuhusu Foundation yake na Epic Open Mic |
Rama Dee na Mapacha |
Mshindi wa EBSS Walter Chilambo akiimba kwenye tamasha hilo.
|
Katika
kuelekea msimu wa sita wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star
Search, kampuni ya simu za mikononi ya Zantel jana imezindua Epiq Open
Mic ikiwa ni nafasi nyingine kwa vijana wenye vipaji vya muziki
kuonyesha vipaji vyao kabla usaili wa Epiq Bongo Star Serach
haujaanza.
Epiq
Open Mic inatarajiwa kuwapa nafasi vijana kujifunza misingi ya muziki
kutoka kwa mmoja wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini,
Marco Chali.
Marco
Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi
ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms.
Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins
kutoka Nigeria na wengine wengi.
Tamasha
hilo la Epiq Open Mic, ambalo ni la bure lilizinduliwa rasmi kwenye
viwanja vya Mwembe Yanga Temeke tarehe 26 ya mwezi huu ikisindikizwa
na wakali kibao wa Bongo flavor kama Diamond Platnumz, Madee,
Godzila, Ney wa Mitego, Mabeste na Mrap.
Baada
ya uzinduzi wa tamasha la Epiq Open Mic Mwembe Yanga tamasha hilo
litaendelea kila jumamosi kwenye makao makuu ya Zantel likiwapa
nafasi vijana kujisajili na kurekod sauti zao.
Vijana
watakaorekodi sauti zao watapigiwa simu na timu ya watayarishaji wa
muziki chini ya Marco Chali pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri
wa namna ya kuboresha muziki wao zaidi.
‘Zantel
imejipanga kutumia fursa hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika
kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na
kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan.
Epiq
Open Mic pia inatarajia kuwapa fursa ya kurekodi baadhi ya vijana
watakaokua na vipaji.
0 comments:
Post a Comment