Tuesday, September 24, 2013

All Hail For The King “He’s Back” – Ujio Mpya wa CPwaa

Fans wake hupendelea kumuita “King of Bongo Crunk”… jina halisi ni Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambaye baada ya ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.
C.P a.k.a CPwaa mwenye tuzo 3 za Tanzania Kilimanjaro Music Awards na Multiple Channel O Africa Music Video Awards nominations anakuja kivingine kabisa mwaka huu. Tarehe 1 mwezi wa October 2013, CPwaa ataachia single yake mpya na ya kwanza kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo iitwayo “Chereko Chereko” yenye mahadhi ya AfroDance imefanywa chini ya studio za ‘De Fatality Music” na producer “Mesen Selekta” ambaye mwaka huu alichukua tuzo ya mtayarishaji  bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo hii itapatikana kwenye mitandao yote na media zote kuanzia tarehe moja October.
CPwaa ambaye amesaini mkataba mnono na Universal Music group vile vile anategemea kuachia single nyingine mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo amewashirikisha mafahari wengine wawili kutoka Afrika. Single hiyo ya kimataifa iitwayo “Cross-Borders Therapy” imekutanisha wakali kutoka mashariki,magharibi na kusini mwa Afrika. CPwaa amemshirikisha “DBlack” kutoka Ghana, DBlack ni moja ya wasanii wakubwa wa Hip Hop Afrika ambaye ana tuzo nyingi ikiwemo zile za Channel O.Kwa upande wa Afrika ya kusini CPwaa amemshirikisha “Hip Hop Pantsula” a.k.a HHP kwenye nyimbo hiyo hiyo ya Cross Borders Therapy.HHP ni mmoja ya MaMC wakali kutoka bondeni mwenye tuzo nyingi ikiwemo ya MTV Base. Nyimbo hii itakuwa ya kwanza Afrika ambayo imekutanisha wakali kutoka mashariki ,magharibi na kusini ( The first East,West and South African Hip Hop Collaboration in History).Nyimbo hii pia imefanyika chini ya producer Mesen Selekta pale  “De Fatality Music” Studio.
Kifuatacho baada ya nyimbo hizi kutoka ni video zake ambapo Chereko Chereko itafanyiwa Tanzania na Cross Border Therapy kufanyika nchini Afrika ya kusini. Kwa wale mashabiki ambao watakuwa na kiu ya wimbo wa Cross Border Therapy ambao utatoka mwakani wataweza kuupata wimbo huo kupitia iTunes,Amazon, Spotify na digital store zingine bila kusahau mtandao wa “The Kleek” kwa wale watumiaji wa smartphones za Samsung na Androids.
Asanteni sana na tuendelee kutoa support kwa wasanii wetu na muziki wetu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support