aka FFU ghaibuni
“The
Golden Voice of East Africa”
Ngoma Africa band yenye mvuto wa ajabu ! na maelfu ya washabiki barani ulaya !
inafananishwa kuwa muzimu wa muziki wenye nguvu !
Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band,ni bendi
ya kwanza ya kiafrika iliyojiwekea nafasi ya pekee katika nyoyo za washabiki
uko ughaibuni.
Bendi hiyo ambayo imetajwa kuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumia
muziki wake kutoka uswahilini kama daraja la kuwafikia washabiki wake katika kona zote duniani,pia imetajwa na
vianzo vya habari vya kimataifa
kuwa mdundo wa mziki wake umekuwa
ni urimbo unao wanasa na kuwatia kiwewe washabiki, popote pale duniani.
Bendi
ya Ngoma Africa band aka FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani
ilianzishwa mwaka 1993 na mwanzilishi kwake mwanamziki Ebrahim Makunja
almaarufu pia kwa majina kama Ras Makunja kamanda wa FFU,Mtawala wa
himaya ya Anunnaki Empire "ambaye pia ndiye mtunzi,mwimbaji na kiongozi
wa
bendi hiyo,bendi hiyo ina utajili wa wanamziki wenye vipaji baadhi yao
wakiwemo
mpiga solo gitaa Christian Bakotessa aka Chris-B aka “Mshenzi” wa solo
gitaa
ambae pia yupo katika safu ya uimbaji,Wengine ni Matondo Benda,Aj
Mbongo na Saidi Jazbo Vuai
wapiga bass gitaa ,Jonathan Sousa aka “Jo Jo” (Drum),wapo akina dada
FrolaWilliam,Jessica
Oyah na Bedi Beraca aka Bedi Bella,bendi hiyo maarufu ina wanamziki
takriban
kumi ,bendi hiyo pia imezungukwa na wataalamu akiwemo Bw.Mfundo Peter
Mufundo,ambaye ni mtayarishaji msaidizi wa mziki
Ngoma Africa band ni bendi iliyo pachikwa majina mengi mengi ya utani au
usanii kama vile FFU, Mzimu wa Muziki, Wazee wa kukaanga mbuyu, majina ambayo
bendi hiyo haiwezi kuyakwepa ! Jina
lingine ambalo lilikua gumu kwao kulikubali ni
“Watoto wa Mbwa” bendi hiyo ilibandikwa jina hilo na baadhi ya wadau wa
mziki, kuwa nyimbo zao ni sawa vitisho
vya mbwa wanao bwaka katika kila sekta na kugusa nyoyo za walio wengi !
Ngoma
Africa band imefanikiwa kufyatua CD nyingi ambazo nyimbo zilizomo
katika santuri hizo zinatawala anga za redio za kimataifa..na
kulitangaza kwa
kasi kubwa jina la Tanzania kanji ya muziki , baadhi ya nyimbo zao ni
pamoja “Rushwa
ni adui wa haki” , Album “Mama Kimwaga”,Single CD “Apache wacha Pombe” ,
CD “Jakaya
Kikwete 2010”,CD "Miaka 50 ya uhuru" na CD Bongo Tambarare na Uhuru wa
habari, ambazo zote ni Utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras
Makunja wa FFU,mjeshi wa ambaye kufanya nae kazi inataka uwe na tabia za
ki
FFU, yaani uwe tayari tayari wakati wowote kwenda kutumbuiza hata ikiwa
katika
nchi za vita ! Na mdundo anautaka yeye lazima uwe na mwendo wa kasi na
magitaa
Lazima yalie milio ya kushambulia mashabiki katika ulingo wa dansi,
mdundo
ambao umepewa jina “Extra Ordinary” Bongo Dance mdundo ambao umefanikiwa
kuwateka na kuwanasa na kuwatia kiwewe watu wengi katika kila kona
duniani,
Wasikilize katika website yao at www.ngoma-africa.com au pia www.reverbnationa.com/ ngomaafricaband
ambayo mpenzi au mshabiki anaweza ku log in na kujumuika nao kama mwanachama wa bendi hiyo.
Ngoma Africa band inaonekana kuwa na mfumo tofauti sana ! Kuwa washabiki wanasauti kubwa ya kuweza kulazimisha maonyesho kuliko uongozi wa bendi !? Mashabiki mara nyingi wamekua tishio hadi kwa
maporomota na waandaaji wa maonyesho makubwa ya mziki…kama bendi ya Ngoma Africa haikualikwa au kupangwa katika ratiba ya onyesho
Fulani basi wapo tayari kususia onyesho hilo…au pengine wakalivunja !
Tena washabiki hao wa umri wa
lika na mataifa mbali mbali hawaoni wala hawasikii kitu kingine chochote mbele
Bongo dansi la Ngoma Africa band aka FFU,ukipenda waite
“Watoto wa Mbwa” au "Anunaki Elien" viumbe wa ajabu kutoka sayari majina yote size yao !
Maporomota au waandaaji wa maonyesho mengi ya mziki huko ughaibuni wanalazimika Kuandaa ulinzi wa kutosha mara tu wanapoialika bendi
hiyo kushiriki katika maonesho yao....hapa ndipo vianzo
vingi vya habari vya ndani na nje ya nchi
vinapofika katangaza kuwa FFU wa Ngoma Africa band “jino kwa jino” au “Jicho kwa Jicho” na
washabiki .
wasikilize katika tovuti yao www.ngoma-africa.com
pia unaweza kuwasiliana nao at contact@ngoma-africa.com
0 comments:
Post a Comment