Amesema kuwa kuachia ngoma hiyo kumekuja ikiwa ni dhahiri
kuitikia wito wa Serikali na Bodi
yake ya Utalii kwamba kila mzalendo
ana jukumu la kuhakikisha utalii wa Taifa la Tanzania unasonga mbele,
naye hajasita kuitumia fursa na haki yake hiyo ya msingi kwa kutumia
rasilimali zake (kipaji alichonacho) kukuza utalii wa Taifa.
Ameongeza kuwa ameshuhudia juhudi za Taifa katika kuutangaza utalii
na vivutio vyake ambavyo ni adimu kupatikana kwingineko duniani kupitia
mabango ya viwanja vya Ligi ya soka la Uingereza na kupitia watu
mbalimbali maarufu duniani nao waka zuru vivutio hivyo wakifaidi
maandhari safi.
Amechagiza kuwa utalii si kwa wageni tu bali pia ni kwa wananchi
wenye nchi kufaidi vilivyo vyao kwa kufanya utalii hivyo amehamasika na
mpango huo naye ameamua kuzama kupitia fani na kuwa amsha wananchi
kufanya utalii wa ndani.
"Kwanza kabisa nawakubali TANAPA" Alisema na kisha kuongeza "Kiukweli
sijalipwa kufanya kazi hii. Kwa sababu mie ni mkongwe katika fani
nilikaa chini nikafanya tathimini na kuandika nilivyo vifanyia tathimini
kuhusu utalii. Najua hata wadau wenyewe wakisikiliza watakubali na
nimewapa ruksa kuutumia wimbo huu kwenye shughuli zote za utalii kwani
najua ni kwa manufaa ya nchi yangu" Alimaliza Bob Haisa.
Usikilize wimbo wake hapa
0 comments:
Post a Comment