Friday, September 12, 2014

Alikiba avunja rekodi ya downloads katika Mkito.com

Nyimbo mbili za Alikiba zimefanikiwa kuongoza kama nyimbo zinazopakuliwa kwa wingi katika tovuti ya Mkito.com.  Wimbo uliotokea kupendwa zaidi wa Mwana ulipanda hadi nafasi ya kwanza ndani ya masaa 12 baada ya kuzinduliwa  Julai 24 mwaka huu.
 
Mpaka sasa “Mwana” ya Alikiba imeendelea kuwa wimbo uliopakuliwa zaidi tangu kuanzishwa kwa Mkito.com mwezi Mei mwaka huu. Wanamuziki wengine wanaofanya vizuri  ndani ya Mkito ni Fid Q, Vanessa Mdee, Young Killer, Diamond Platnumz, Linah, Rich Mavoko, ROMA, Mkubwa na Wanawe.
 
Alikiba amesema “Nina furaha kubwa sana hivi sasa, napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote kwa upendo, kunikubali na kwa kuunga mkono muziki wangu na pia nafurahia kuona ukuaji wa muziki wetu ndani na nje ya nchi”
 
Mkurugenzi wa Mkito Sune Mushendwa amefafanua kuwa “Ni kitu cha kawaida ulimwenguni kwa wanamuziki kutangaza kazi zao kidigitali kupitia makampuni ya usambaji mtandaoni, kuziuza kazi zao pande zote za dunia na kujiongezea kipato”
 
Sune aliongeza kusema “Nchini Tanzania huduma hii haikuwepo kwa sababu teknolojia ya kidigitali ilikuwa haijasambaa vya kutosha lakini kwa hivi sasa hali inabadilika kwa kasi, kufuatia kusambaza kwa huduma ya broadband kupitia mkongo wa taifa ambayo imepelekea kuongezeka kwa huduma za usambazaji mtandaoni mojawapo ikiwa Mkito.Com ambayo itahakikisha inatangaza kazi za wasanii kidigitali na kuwafikishia maslahi wanayostahili.”
 
Katika muendelezo wa ujio wake mpya, mwanamuziki Alikiba anatarajiwa kutumbuiza katika moja ya matamasha makubwa barani Afrika litakaloanza Septemba 26-28 2014 akiwa pamoja na wanamuziki Nicki Minaj, J Cole, Kid Ink, Fally Ipupa, D’Banj ikiwa ni sehemu ya wasanii wa ndani na nje ya Afrika.
 
Jiunge na Mkito
Website: www.mkito.com
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support