“Nikiwa na umri mdogo sana nilijikuta napenda kusikiliza
muziki na hata nikiwa shuleni mwalimu aliyeni vutia sana alikua wa michezo na
muziki namkumbuka Mwl. Julieti aliyewahi kushika nafasi hiyo pale Mitindo shule
ya msingi. Siku za ijumaa tulitolewa mapema shuleni ili kujiandaa na swala ya
ijumaa, kiukweli nilikua nawahi nyumbani kwa lengo la kusikiliza muziki wa
mwambao kupitia RTD walikua wakipiga muziki huo muda wa saa saba mpaka saa
nane.Mmoja kati ya watu walionivutia sana katika kipindi cha muziki wa taarabu
ni Bi Shakila ambae mara chache tu ndo kipindi kilimalizika bila wimbo wake
kwenda hewani, uimbaji wake ulitukuka sana nafsini mwangu hapo nilikua mdogo
kama miaka 12 hivi na tayari nilitamani kuimba muziki wa taarab ila kwakua
nilikua mdogo, nilitumia shauku hiyo kwa kushiriki uimbaji wa Qaswida madrasa
na kutumia vionjo vya Bi shakila katika kunakshi Qaswida jambo lililonifanya
niwe star kwenye madrasa. Nilipomaliza shule ya msingi ilikua ndo mwisho wangu
pia kushiriki madrasa na Qaswida zangu zilitulia kwa muda mpaka nilipojikuta
naibukia kwenye muziki wa asili ya kisukuma baadae rap miduara na bongo flava
ambapo umaarufu wangu ulibebwa na miduara zaidi kutokana na single ya Nipe
mgongo ambayo ilipelekea niingia kwenye orodha ya waimbaji wa muziki wa pwani
na kunipa nafasi ya kukutana na wakali wengi wa muziki wa pwani wakongwe na
wapya , Nakumbuka siku ambayo sikuamini maskio yangu pale nilipopokea simu
kutoka zanzibar sauti nzito iliskika. .Haloo Asalaam alaikum, niliitikia kisha
baada ya maelezo nilitambua naongea na Yusuf Chuchu 'mungu amrehemu' na habari
aliyonipa ndo ilinifanya nisituke zaidi kwani ni mwaliko wa kupiga show ya
pamoja na Bi Shakila Ooh iliku siku nzuri sana kwani nilijikuta nakumbuka mengi
sana na sikua na pingamizi na safari ya zanzibar ikaanza kutoka dar mpaka
zanzibar Nilifika zanzibar na shauku yangu kubwa ilikua kumuona Bi Shakila
ambae tulikutana nae ndani ya Chuchu Fm hapa ilikua kati ya 2008 na 2009
kwakweli nilisikia sauti ya Bi shakila akiimba huku nikimuona live wakati
akifanyiwa mahojiano na hapo nilikumbuka mbali kwani licha ya umri wake kupea
bado sauti ilikua ileile sikusubiri tena bali alipomaliza zamu yake ya kuongea
tu nikamfata na kumnong'oneza ombi langu. .Tafadhali mama naomba unifundishe
kuimba, aliposkia neno lile alitabasam kidogo akanambia tutaongea kisha
tuliendelea na mahojiano na zamu yangu ya kuhojiwa ilifuata baada ya joan,
spider na wengine tuliokuanao pale redioni, muda ulipotimia tulienda ukumbini
na show ilikua moto sana, tulimaliza na kubadilisha namba wote tuliokua
tukitumbuiza pale ukumbini .siku iliyofuata ilikua jumapili jioni tulipokutana
maeneo ya Forodhani na baada ya kupata urojo mishikaki ya samaki, nyama na
pweza kwa ndizi na chips.
Mbali na mapochopocho hayo jumapili, hiyo ndo siku
tuliyokubaliana kufanya kazi ya pamoja siku na saa ambayo hatukuipanga,
tulitawanyika huku nikifikiria kazi ya kushirikiana na Bi Shakila je iwe taarab
mduara au reggae? Sikupata jibu, miaka ikapita huku tukiwasiliana mara kadhaa
mpaka valentine day ya mwaka 2013 pale nilipoalikwa tena na ndugu yangu Richard
Luhende kwenda kutumbuiza morogoro sambamba na Bi Shakila tulipokutana
alinikumbusha Vp mpango wetu tatizo letu wasanii twapanga mengi halafu
hatutekelezi nilimuelewa alichomaanisha nikamjibu Mungu hajapanga siku
yetu. Tukapiga show asubuhi tukaagana kwa kunywa chai pamoja mimi nikarudi
misungwi na Bi shakila akarudi dar”.Bob Haisa
Itaendelea.....
0 comments:
Post a Comment