Breaking News

Monday, October 20, 2014

New Video : Hemedy PHD & Gelly Wa Rhymes - The One

Official Video ya wasanii HEMEDY PHD na GELLY WA RYHMES. Nyimbo inaitwa THE ONE,audio imetengenezwa na SEI wa SEI RECORDS. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Muongozaji ni Msafiri Shabani.
Read more ...

New Music : Mad Ice - Everything I Do

Mad Ice ni msanii aliyezaliwa nchini Uganda na kuishi Tanzania kwa muda mrefu ambapo aliaanza rasmi kazi yake ya muziki na kutoa albam yake ya utambulisho iitwayo BABY GAL (2003, Chini ya Miikka Mwamba). Msanii huyu wa Afro-Soul baada ya album hiyo alihamia nchini Finland ambapo aliendeleza kazi pamoja na producer Miikka Mwamba na studio nyingine nchini humo na kutoa nyimbo nyingi zilizoshika chati tofauti duniani kote zikiwemo Maneno, Mapenzi Sumu na Te Amo.

Hii ni Single mpya kabisa ya Mad Ice inaitwa EVERYTHING I DO na imefanyika Sonic Pump Studios, Finland chini ya producer DJ Hermanni.
Read more ...

Saturday, October 18, 2014

Coming Soon : Mad Ice - Everything I Do

Mwanamuziki Mad Ice amerudi Tanzania kutoka nchini Finland ambapo ametoka kurekodi single yake mpya EVERYTHING I DO chini ya producer DJ Hermanni kwenye studio ya kimataifa ya Sonic Pump Studios (http://www.sonicpumpstudios.com/). Mara nyingine huwa inatosha kuangalia mandhari ya studio kujua kuwa kazi zinazotoka huko lazima ziwe na kiwango cha kimataifa. Tazama picha hizi za studio halafu tusubiri kusikia mapishi yake Jumatatu tarehe 20 Oktoka.
Read more ...

Ujio wa Angel Benard

ANGEL BENARD ni jina ambalo limekuwa likisikika kwa miaka kadhaa sasa kwenye ulimwengu wa muziki wa gospel. Angel Benard mwenye miaka 25 hatimaye sasa anaachia album yake NEW DAY kwenye mfumo wa digitali kupitia Mkito.com. Watu wengi wamekuwa wakisubiri kusikia nyimbo zake za zamani lakini haikuwa rahisi kuzipata. Album hii ni album ya 3 ya mwana dada huyu mwenye sauti ya maajabu. Ni wasanii wachache sana wa muziki wa gospel ambao wamefanikiwa kuvusha nyimbo zao zikapendwa na wapenzi wa gospel pamoja na wapenzi wa muziki wa bongo flava, RnB n.k. na mwimbaji huyu ni mmoja wapo.

Katika kuitambulisha album hii Angel Benard ataachia wimbo mmoja kila siku ya Alhamis kwa wiki 10 mfululizo. Wimbo wa kwanza utatoka tarehe 23 October na unaitwa NEED YOU TO REIGN ukiwa katika minodoko ya Reggae.
Read more ...

New Video : The'Kisser Strawberry - Umependeza

Msanii anayechipukia The'kisser Strawberry (Instagram@thekisser_strawberry) mwenye asiri ya mwanza hatimaye amefanikiwa kuachia rasmi video ya wimbo wake wa 2 uitwao UMEPENDEZA. 
Msanii huyo aliachia rasmi video hiyo kupitia runinga ya EATV/Ch5 katika kipindi cha 5Seleck na kisha kuwaaidi mashabiki wampokee vizuri akiwa kama msanii mpya pia wasubilie mengi kutoka kwake....
                 Video hii imefanywa katika kampuni iitwayo CreativeMinds Tz chini yake Director Eddie.
Read more ...

New Video : Angel Benard - Need You To Reign

Angel Benard ameachia video ya wimbo wake mpya 'Need you to reign' ambao unapatikana katika album ya 'New Day' audio yake itatoka Rasmi tarehe 23 October.Itazame hapa
Read more ...

Friday, October 17, 2014

New Music : Mkubwa na Wanawe - Inooh

Wimbo mpya kutoka kwa Mkubwa na Wanawe ambao ni kati ya nyimbo zilizopo kwenye collection ya NISEME. Wimbo huu inaitwa INOOH. Mkubwa na Wanawe ni wansanii ambao kwa muda mfupi sana wameweza kuonekana katika majukwaa makubwa na kuwa na mafanikio makubwa sana kimuziki wakiwa chini ya usimamizi wa Mkubwa mwenyewe Saidi Fela. Fela ni meneja ambaye amesimamia na kuwatoa wasanii na makundi kama Juma Nature na Wanaume. Pata wimbo mpya kabisa kutoka kwa Mkubwa na Wanawe kupitia Mkito.com sasa.

https://mkito.com/song/inooh/3014
Read more ...

New Music : Hisia - Mawazo (With Lyrics)

Msanii Hisia ambaye aliiwakilisha vyema sana nchi yetu katika mashindano ya Tusker Project Fame mwaka jana anakaribia kuachia wimbo wake mpya uitwao GIVE ME A CALL hapo tarehe 25 Octoba katika show ya live. Katika kuusubiri wimbo huo tujikumbushe track yake ambayo imeshika chati nchini Kenya kwa wiki 6 mfululizo iitwayo MAWAZO. Wimbo huu pia unapatikana kama acapella, yaani vocal tu, ili wapenzi wake tusikie ni kwanini Hisia aliweza kufanya vizuri vile kwenye mashindano ya Tusker Project Fame.

Kwa wale wote watakao taka kufika kwenye show yake itafanyika tarehe 25/10/2014 Alliance Francaise kuanzia saa moja jioni.

Read more ...

New Video : Timbulo - Nakumiss Miss

Timbulo ameachia video ya wimbo wake mpya "Nakumiss Miss" Itazame hapa
Read more ...

New Video : Yemi Alade - Kissing

 
Yemi Alade ameachia video ya wimbo wake mpya unaojulikana kama "Kissing" Itazame hapa
Read more ...
copyright © 2012-2014 Mashaka Kisusi