Wednesday, March 5, 2014

Bob Haisa aeleza sababu ya kufanya wimbo wa 'Safari ya Utalii'

Amesema kuwa kuachia ngoma hiyo kumekuja ikiwa ni dhahiri kuitikia wito wa Serikali na Bodi
yake ya Utalii kwamba kila mzalendo ana jukumu la kuhakikisha utalii wa Taifa la Tanzania unasonga mbele, naye hajasita kuitumia fursa na haki yake hiyo ya msingi kwa kutumia rasilimali zake (kipaji alichonacho) kukuza utalii wa Taifa.

Ameongeza kuwa ameshuhudia juhudi za Taifa katika kuutangaza utalii na vivutio vyake ambavyo ni adimu kupatikana kwingineko duniani kupitia mabango ya viwanja vya Ligi ya soka la Uingereza na kupitia watu mbalimbali maarufu duniani nao waka zuru vivutio hivyo wakifaidi maandhari safi.

Amechagiza kuwa utalii si kwa wageni tu bali pia ni kwa wananchi wenye nchi kufaidi vilivyo vyao kwa kufanya utalii hivyo amehamasika na mpango huo naye ameamua kuzama kupitia fani na kuwa amsha wananchi kufanya utalii wa ndani.

"Kwanza kabisa nawakubali TANAPA" Alisema na kisha kuongeza "Kiukweli sijalipwa kufanya kazi hii. Kwa sababu mie ni mkongwe katika fani nilikaa chini nikafanya tathimini na kuandika nilivyo vifanyia tathimini kuhusu utalii. Najua hata wadau wenyewe wakisikiliza watakubali na nimewapa ruksa kuutumia wimbo huu kwenye shughuli zote za utalii kwani najua ni kwa manufaa ya nchi yangu" Alimaliza Bob Haisa.
Usikilize wimbo wake hapa
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support