Sunday, September 22, 2013

BOB HAISA-DAMU YA AFRIKA (LYRICS)

Mmmh. Amka afrika amka ulinde damu yako isimwagike hovyo hovyo. .
Hivi! Kwanini . . Damu ya Africa inakosa thamani yamwagika hovyohovyo. .
Hivi mpaka lini mateso ya mwafrica njaa na maradhi twaongezewa silaha.X2
 Afrika ya kale ilikua shwari, leo afrika dimbwi la damu,
Africa ya kale ilikua nzuri, leo afrika yageuzwa jehanamu,
Wanaoanzisha vita ni wababe kwanini afrika? 
Ila wahanga wa vita ni wanyonge 'Kwanini' afrika?'' 
Wanaoanzisha vita ni wakubwa 'kwanini afrika?' 
Ila wahanga wa vita ni wadogo kwanini afrika? 
Inauma sana unapomuona mama akiwa na mwana katikati ya vita, 
Kunawalemavu wazee na watoto watamudu vipi kukwepa makombora, 
Hebu fikiria mama mjamzito kushikwa uchungu katikati ya vita,
Ni huzuni sana kukiona kichanga kikinyonya kwa mama na mama keshakufa kwa vita aeee. 
Kukicha yamwagika 'damu ya afrika'
Kwa mifereji michafu damu ya afrika
 Ya madaraka na mali. .'damu ya afrika'
 Yaani imekosa thamani kabisa 'damu ya afrika'
 Hey hiiiiy.afrika ni moja muafrika mmoja lengo letu moja kujikomboa, 
Tunapochinjana kwa mikono yetu jeshi letu dogo lazidi dhonfika, 
Waliotutenga wao walingoja, Uishe kabisa wetu umoja ili watuchape mmojammoja.
Walishindwa tukiwa pamoja,Afrika tuungane .
Maathanga othe aafrika tugurane tuoke kindu kimwe twidime.
Turudishe umoja wetu waafrika yenye nguvu, tusimame tulinde damu yetu.
Mali zisiwe chanzo afrika unite, Siasa isiwe chanzo afrika unite.
Dola zisiwe chambo afrika unite, Madini yasiwe chambo afrika unite.
Aafrikaee afrikaee afrika uniteX2
 wana wa afrika tunakwenda wapi ? 
Hata ardhi tuliyopewa na mungu imekua chambo kutuangamiza sisi wenyewe.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support