Monday, January 6, 2014

WIMBO WA BOB HAISA 'WIBISILENO SEBHA' WAZUIWA MTANDAONI

Akizungumzia suala hilo Bob haisa amesema kuwa alipanga kuuachia wimbo wake huo tarehe 01/01/14,
lakini alisikitishwa na habari alizozipata kuwa baada ya kuwekwa wimbo huo mtaandaoni ulizuiliwa moja kwa moja kwamba hana ruhusa ya kuweka wimbo huo kwani wimbo huo beat iliyotumika ni ya R. Kelly.
"Kwakweli lilikuwa jambo la kuniamsha sana pale nilipoambiwa kwamba wimbo wangu wa Wibisileno sebha umegoma kuwa uploaded mtandaoni, nilikuwa ndani ya basi naelekea Ishokela huku nikiwa nimeacha maelekezo kwa afisa habari wangu kuwa wimbo uwekwe mtandaoni tarehe 1 kama zawadi ya mwaka 2014, ndipo nilipoambiwa kuwa wimbo umegoma kupakiwa mtandaoni kwakuwa ni miliki ya mwanamuziki R.kelly. Nilijifunza kitu katika ulinzi wa kazi zetu kama wasanii . Hata hivyo nitajitahidi kufuata taratibu zaidi ili R. Kelly aniruhusu kutumia beat yake katika wimbo wangu uitwao WIBISILENO SEBHA".Alisema Bob Haisa
Pia Bob Haisa amezungumzia maana ya Wimbo wake mpya wa Mazongo Zongo
" Ni mtindo wa uchezaji ulioibuka kwa kasi hivi karibuni maeneo ya Usukuma ambapo wanawake hujitoa fahamu na kuvua nguo kama ilivyo kwenye baadhi ya Club za usiku mijini. mtindo huu ni hatari kwa  ustawi wa sanaa ndo maana kwenye wimbo wa mazongozongo nimekemea mtindo huo kama si kuubadilisha kabisa". aliongeza Bob Haisa
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support