Wednesday, October 22, 2014

New Music : Mwana FA Feat. Alikiba - Kiboko Yangu

Sote tumeusubiri kwa hamu na sasa wimbo mpya kabisa wa Mwana FA na Alikiba umewasili rasmi. Baada ya Mwana FA kutoa wimbo wa Mfalme live katika tuzo za KTMA 2014 msanii huyu ameungana na mfalme wa bongo flava yaani Alikiba ili kuwaletea mashabiki wake kazi nyingine kali. Producer wa wimbo huu si mwingine bali ni Marco Chali wa kutoka MJ Records ya jijini Dar Es Salaam. Katika kuurekodi wimbo huu kumekuwa na matoleo manne tofauti ambayo wadau walikuwa wakisindwa kuamua ni upi wa kuachia kwa kuwa zote zimesimamia kucha. Mwana FA na kampuni ya LifeLine ambaye yeye pia ni mkurugenzi wameamua kuuachia wimbo huu moja kwa moja kupitia Mkito.com ili kuhakikisha unawafikia wapenzi wake wengi zaidi na kuhakikisha kuwa kuna maslahi yanapatikana katika kazi hii. Pakua wimbo huu mpya kabisa sasa upate flava kali.https://mkito.com/song/kiboko-yangu-ft-ali-kiba/3036
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support