Monday, July 8, 2013

HII NDIO NDEGE YA ASIAN AIRLINES ILIYOPATA AJALI


Kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha San Francisco nchini marekani
kumetokea ajali ya ndege iliyohusisha ndege moja ya Asian Airline ambayo iilkuwa na abiria wengi kutoka bara la Asia ambapo mpaka ajali imetokea watu walioweza kujulikana uraia wao ni wachina 141 ambao kati yao kuna wanafunzi wa high school 32 wakitokea China kuelekea Marekani kwenye summer camp, abiria 77 ni wakorea, 61 Wamarekani, Wahindi 2 na taarifa zaidi ni kwamba watu karibu 180 wamekimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha na waliofariki hadi sasa ni watu wawili tu. Kutokana na maelezo ya maofisa wa Asian Airline, ndege yao haijapata crash hii kutokana na tatizo la injini bali kuna tatizo lingine ambali bado halijajulikana kwa sababu hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa, kwenye mabaki ya ndege hiyo wataalamu wameweza kupata kifaa kinaitwa black box ambacho hurekodi mambo yote ya safari ya ndege, hivyo basi itasaidia katika kupata majibu juu ya sababu ya ajali hii.
VIDEO YA JINSI ABC NEWS WALIVYO REPORT HII AJALI


Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support