Friday, October 18, 2013

FID Q FT. JUMA NATURE-SIRI YA MCHEZO (LYRICS)


Fid-q-siri-ya-mchezo

Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na  umuhimu kihivyo… stimu  zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../  sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa  #teamMabiiitoz  /
Achana na  power window.. sijui  rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko?  Star ishi simple/   sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui  kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa  ukuone hauna ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za  harakati ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/  na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji  kama  Kubanda eti unachana kigumu/  kisa  track ikivuma sana kwenye chati  haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../  baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../  najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../  inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
‘’Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni  wahuni  hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../  huo ni utumwa pia/Unafanya  vijana  wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..


CHORUS:  ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2
Siri ya mchezo naijua  mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2


VERSE 2:
Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma/ wakati SIASA kila mara ukiwa unang’ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/ KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/
tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ‘  demu wa mtungo ‘ wanamuiita CHA WOOTE/’’ HANGOVER .. ‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote /Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/ ‘’na  gari bovu..’’  halisukumwi kwa kukaa ndani yake/
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../  je  Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? /
hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/
na daily tunafeli sababu ya  POLITICAL institutions/
CIVILIZATION  imeadvance sasa wanatuua economically../
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/
Kuusaka ukweli  ni  sawa na kumenya kitunguu/
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/
Ukishafika kwenye kiini  niambie nini utagundua..?
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support