Saturday, November 9, 2013

BOB HAISA-MEZA YA WANANDOA (LYRICS)


Enyi mlio katika ndoa nisikilizeni ninayosema
 leo nasema juu ya lile somo linalohusu wanandoa
 tuijadili ile meza meza ya wanandoa 
tuzungumzie ile meza meza ya wanandoa
 Meza ile imepambwa vyema 
mapochopocho mbalimbali
 tena inawavutia wengi 
hata wasio wanandoa 
aloiandaa keshasema 
hiyo ni meza ya wanandoa 
hakuna ruhusa kuzamia 
hiyo ni meza ya wanandoa 
yee baba nawe mama 
tuijadili ile meza meza ya wanandoa
 tuzungumzie ile meza meza ya wanandoa
 Chakula kabla ya kwenda mezani kinapashwa moto
 na pale mezani pia kitunzwe kwenye kitunza joto 
msilishane chakula kilichopoa kwenyemeza ya wanandoa hata kama kiporo chakachua kinapashwa moto
 na pale mezani pia kitunzwe kwenye kitunza joto 
Kila mmoja na chombo chake anasema anachopenda amwambie mwandani wake ampakulie anachopenda kama moyo unapenda kuku amkatie anapopenda iwe ni shingo ama papatio amkatie anapopenda hata kama moyo ukipenda tembele mpakulie wewe akisema nakula kwanza matunda msogezee wewe wala msione haya kusema niongezee tena ondoa mawazo hasira na chuki ili ushibe vema unapokula kwa tabasamu kwenye meza ya wanandoa utaona chakula kitamu kwenye meza ya wanando meza ile yapendeza inapoandaliwa vema maua na kitambaa cheupe inapambwa vyema mwanga wa mshumaa unamulika mapochopochopochopocho eeya.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support