Thursday, November 28, 2013

BOB HAISA-NITHAMINI NIKIWA HAI (LYRICS)

Nithamini nikiwa hai usingoje nife unililie nisfie nikiwa hai nitakapokufa uniombeex2

mwenzako ninaumwa kitandani huji kunitazama wasubiri siku niwe jenezani uje kunililia mwenzako niko hoi kitandani huji kunitazama wasubiri siku niwe jenezani uje kunililia unasubiri habari zangu kupitia gazeti na intanet wakati we nirafikiangu twaishi wote pale mitaa ya kati watakajua uzima wangu kupitia kwenye vyombo vya habari wakati we ni rafiangu twaishi wote pale mitaa ya kati. . tatizo moja kweli kwetu ubize ubize wangu mimi na wewe . .wewe bize na misele mimi bize kitandani wewe bize na michongo mimi bize na maradhi . . Habari za uzushi juu ya kifo changu ndizo zilokuzindua wewe, cha kwanza kukiwaza kabla ya sanda yangu wawaza utatokaje wewe kwenye mazishi yangu wawaza kuendeza . gari zuuri la thamani suti kali ya ghara wanichagulia jeneza zuri upatie picha nzuri . .habari za uzushi juu ya kifo changu ndizo zilokugutua wewe chakwanza kukiwaza kabla ya sanda yangu wawaza utapataje wewe habari za kizushi . . Ulisahaugu kubeba dawa zangu leo umekumbuka kubeba kamera tatu. .nikiwa hai unanikimbia nitakapokufa je utanililia, nikiwa hai unanifukuza nitakapokufa je utanililia nikiwa hai unanipondea nitakapokufa eti wanisifia nikiwa hai unanibania nitakapoufa we wanifagilia maisha ni safari tuendako hatupajui ukiweza kutembea mtazame anaetambaa ukisimama mwangalie aliyelazwa hujafa hujaumbika huruma yako ya leo ni msaada wako kesho ee Mola wapumzishe waliotangulia wape afya njema wanaougulia ee muumba tubariki waja wako. Bob haisa Yes yes.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support