Monday, November 25, 2013

MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND A.K.A FFU WAUTEKA MJI WA BREMEN,UJERUMANI


FFU wa Ngoma Africa Band wameliteka tena jiji la Bremen !

Wamevuna umati wa washabiki wa kimataifa


Bremen,Ujerumani,

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni,usiku tarehe 23 Novemba 2013 walifanikiwa kwa mara nyingine tena
kuliteka jiji la Bremen,kule ujerumani. Kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU alikiongoza jukwaani kikosi kazi chake katika jumba la Ãœbersee-Museum akiwa na matumaini kuwa wanaenda kumbuiza washabiki high class wenye adhi ya kibwanyenye lakini mziki ulipoanza mdundo uliwachanganya washabiki na kuwadatisha akili ! kila mmoja alijimwaga uwanjani !
Ngoma Africa Band walijikuta wapo katika kibarua kama kawaida yao cha kushambulia kwa virungu vya muziki na kufanikiwa kuutapanua uwigo wake
kwa kuwanasa washabiki wengi wa kimataifa.
Bendi hiyo maarufu iliyojiimarisha na kujenga himaya ya kimataifa kwa kutumia
muziki wake,meshatajwa mara nyingi kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya,
bendi ya Ngoma Africa inafanananishwa sawa na kikosi maalumu cha kuzuwia ghasia FFU, pia ina majina mengi ya utani na kiusanii kama vile viumbe wa ajabu  "Anunnaki Elien" n.k ambayo imepewa na washabiki au wapenzi wake,kiongozi wake pia ana majina kama vile kamanda Ras Makunja wa FFU,mtawala wa Anunnaki Empire.
Ngoma Africa band wanasikika at www.ngoma-africa.com











Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support