Friday, December 27, 2013

DANCERS WA BOB HAISA WADAKWA NA POLISI

Ni baada ya show yake iliyofanyika usiku wa Christmas mkoani Geita, Akiongea na Blog hii
Msanii huyo ambaye ni mkufunzi wa mziki nchini amedai kuwa Dancers wake wamekamatwa wakiwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza leo asubuhi.
"Polisi wa wilayani Misungwi wamekuwa wakiniandama sana mpaka inafikia wakati inanibidi kufanya mazoezi usiku ili kuukwepa usumbufu wao", alilalamika msanii huyo.
Pia aliongeza kuwa Sio mara ya kwanza polisi hao kumsakama bila kujua kosa kwani alisha wahi kuandaa tamasha la kutafuta vipaji vya waimbaji chipukizi lakini polisi waliingilia kati na kulivunja tamasha hilo wakati alipewa kibali cha kufanya tamasha hilo na wao kulivunja kwa kudai kuwa halina kibali.
"Nawasihi polisi wajipange kunisapoti kuliko kuniandama, Mimi ni mwakilishi wao leo wananimwagia mboga bila kujua siku moja nami nitamwaga ugali. Misungwi ni nyumbani kwanini wanifanye mkimbizi?"Alihitimisha kwa kutoa wito kwa Polisi hao.
Mpaka sasa Mkufunzi huyo wa mziki nchini yuko mafichoni kwa kuhofia kukamatwa na askari hao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support