Friday, December 6, 2013

NGOMA AFRICA BAND YATOA SALAM ZA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani Ulaya "Ngoma Africa" aka FFU,
Inawatakia kila la heri na fanaka waTanzania wote kwa kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania (bara),Uongozi wa  bendi hiyo unaiombea kila la heri, Serikali ya Tanzania,Wananchi na Taifa la Tanzania.
Katika kusherekea miaka 52 ya Uhuru,Ngoma Africa band inawaombea wadau na wananchi wote popote walipo,kutumia wakati huu  kujikomboa kimawazo,na kuhakikisha kuwa tunajenga na kudumisha umoja,mshikamano na upendo wa kitaifa, ili kuleta maana kamili ya "Uhuru" wa maisha ya Mtanzania.Katika Kusherehekea miaka 52 ya Uhuru, watanzania tunapaswa zaidi kujenga na kuziba nyufa zinazo bobomoa au kujaribu kubomomoa msingi wetu imara wa umoja,Upendo na mshikamano wa kitaifa.
Mungu Ibaraki Tanzania !Mungu wabariki Watanzania !
Mungu Ibariki Serikali ya Tanzania !

Tafadhali pata burudani kamili at www.ngoma-africa.com



Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support