Tuesday, October 1, 2013

USHAURI KWA BOB HAISA

"Hii ni kwa ajili ya mashabiki wangu (Bob Haisa) je? ukipewa nafasi ya kurekebisha mashairi haya ya Wimbo wa
Unisamehe yawe bora zaidi ungerekebisha neno lipi na lipi? Nisaidie mdau niko kwenye maboresho". Bob haisa
Verse 1
Mpenzi wangu napigagoti mbele yako,
Mikono yangu nashika miguuni mwako, 
Ninakuomba fungua msamaha wako 
Kwangu mimi kiumbe dhaifu mwenzako,
Ninajua itakua ngumu kwako 
Kuyasahau yote nilotenda kwako,
Ninajua itakua ngumu kwako
Kuyasahau yote nilotenda kwako
 Ninajua itakua ngumu kwako
Kuyasahau mabaya nilotenda kwako,
Kumbuka yakua mungu husamehe,
Hata wewe inakubidi unisamehe,
Kumbuka yakua mungu husamehe 
Na hata wewe inakubidi unisamehe,
Hakuna binadamu mpenzi aloumbwa akakamilika,
Hakuna binadamu baby asietenda makosa,
 Kiitikio
 Naomba unisamehe kosa nililofanya 
Hakika mi binadamu kukosea nimeumbiwa
Naomba unisamehe kosa nililofanya 
Hakika mi binadamu nastahili msamaha
Verse 2
 Najua kwamba nimetenda kosa mpenzi 
Moyo wako umeingia simanzi,
Japo naumia kuwa mbali nawe mpenzi,
Sintolaumu uamuzi wako wewe,
Ukiamua kunisamehe mpenzi wangu
 Ujue kwamba umeokoa maisha yangu,
Mikononi mwako nimekabidhi moyo wangu 
Ukiutupa utakatisha maisha yangu, 
Mikononi mwako nimekabidhi moyo wangu 
Ukiutupa utakatisha maisha yangu,
Hebu fikiri upya baby ntaishi vipi bila wewe,
Hebu rudisha moyo mpenzi uniokoe maisha yangu,
Kiitikio
Naomba unisamehe kosa nililofanya,
Hakika mi binadamu kukosea nimeumbiwa,
Naomba unisamehe kosa nililofanya 
Hakika mi binadamu nastahili msamaha,

Mpenzi nijutia nafsi yangu kwa yote niliyokutendea 
Najua nimekuumiza sana lakini kwa sasa naomba unisamehe
                                                          
                                                                  
Kiitikio
Naomba unisamehe kosa nililofanya,
Hakika mi binadamu kukosea nimeumbiwa,
Naomba unisamehe kosa nililofanya 
Hakika mi binadamu nastahili msamaha,

Bofya Hapa kusikiliza wimbo kamili http://old.hulkshare.com/wt179b11o64g



Share:

7 comments:

  1. Ngoma ni kali sana kikubwa labda amtafute msanii wa kike wamake collable

    ReplyDelete
  2. mi naona mashairi yako poa

    ReplyDelete
  3. mashairi yako powa kikubwa jipange kutengeneza video yake

    ReplyDelete
  4. wakukaya tengeneza track nyingine maana ukipunguza au kuongeza mashairi utaiaribu kaka jipange kwa kitu kipya......naikubali ngoma yako ya nikikuonaga sarutii....

    ReplyDelete
  5. iko sawa bro iache hivyo hivyo

    ReplyDelete
  6. mashairi yako poa mno yasibadilishwe

    ReplyDelete
  7. hakuna kipya chakuongeza

    ReplyDelete

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support