Wednesday, June 25, 2014

Bob Haisa atimiza mwaka mmoja tangu aanze kutoa ngoma mpya kwa kila mwezi

 Mwanamuziki Bob Haisa leo ametimiza mwaka mmoja tangu aanze kuachia nyimbo zake mtandaoni kwa kila mwezi,akiongea na blog hii alisema kuwa "Leo ni siku muhimu kwangu kwani mwaka mmoja unatimia tangu nianzishe rasmi utaratibu wa kuachia ngoma zangu kupitia mitandao, nakumbuka wimbo wa amechoka wakukaya video ndo ulifungua dimba kwa kuingia mtandaoni kwa 'TASHTITI" nyingi, licha ya kwamba wimbo huu uliwekwa mapema na director Louis Bwenge. Tarehe ya leo ndo ulisambazwa rasmi na kuwafikia mafans wangu wengi hali iliyoamsha ari zaidi na kunifanya nitangaze rasmi kwamba kila mwezi nitaachia wimbo mmoja zoezi ambalo limefana vyema ndani ya mwaka mzima. Zaidi ya nyimbo kumi na mbili zimekwenda hewani na zimepokelewa poa sana na ma Djs na wanahabari pamoja na mashabiki na wapenzi wa muziki wangu,hii imekua njia nzuri na rahisi kwangu kuwafikia watangazaji wa Radio na Tv mbalimbali kwakua wanazipata ngoma kwa muda muafaka na kuzitendea haki.
Changamoto kadhaa nimekutana nazo lakini hazikuathiri zoezi hili kwani malengo hayajakwama na ndo kwanza safari inaanza, niwe muwazi kwa kuwashukuru wote walioniunga mkono katika zoezi hili endelevu linalohitaji ushirikiano na uungwaji mkono pia napenda kuwahakikishia wadau wangu kwamba kila tarehe 15 ya kila mwezi nitaendelea na zoezi la ngoma mpya moja baada ya moja. Ahsanteni Sana" Bob Haisa Yes.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support