Monday, August 11, 2014

Bob Haisa aanza ku-shoot video ya Lamsondo


Mwanamuziki kutoka Mwanza,Bob Haisa ameanza ku-shoot video ya wimbo wake mpya 'Lamsondo' akiongea na blog hii alisema "Jun 15, 2014 Niliuachia rasmi wimbo Lamsondo kupitia mitandao mbalimbali ndani na nje ya nchi kisha ikafatia remix yake Aug 1, 2014 ambayo pia ilisambaaa kwa kasi sana lakini kama haitoshi Aug 3, 2014 niliingia location ndani ya fukwe za Shafiq Beach kufanya video yake ambapo watu kibao wakiongozwa na Peace Film Production walisimama kunisupport.

Bob haisa akiwalocation na warenbo washiriki ndani ya maji.


Warembo zaidi ya 15 walishiriki pamoja na wanaume wakali wa miduara kutoka Mwanza. Location ilipambwa, wengi waliofika Shafiq Beach Jumapili hiyo ya tarehe 3 na walishindwa kujizuia na kujiunga kupiga duara. Nathubutu kusema huu ndo wimbo wa mduara uliofungua safari yangu ya kurudia style ya mduara ambayo kwa muda nilijitenga nayo.
Bob haisa akiwa pamoja na baadhi ya washiriki na wadau wa video ya lamsondo

Kuanzia audio iliyoandaliwa na producer king fenya wa Mbunda Records mpaka video zimekidhi kiwango kinachoendana na uhitaji wangu pamoja na mashabiki na wapenzi wa muziki wangu hususani wanamduara wenzangu. Hebu fungua macho na maskio usikie na uone ujio wangu mpya kwenye miduara lakini pia nawapongeza wale wote waliojitokeza baada ya ukimya wangu nipokeeni tuburudike."
 Hawa wawili ni director ken akiwa na msaidizi wake jina Nestor
 King Fenya producer wa audio ya lamsondo akiwa pamoja na mr Armon mkurugenzi wa peace film production walio simamia mzigo wa vdeo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support