Tuesday, August 19, 2014

Video : Mkasi | SO9E09 with Dudubaya

Wengi mnamjua kama Dudu Baya, ila jina halisi ni Godfrey Tumaini! Mzaliwa wa Mwanza na mmoja wa watoto 13, Godfrey ana historia ndefu yenye kupanda na kushuka kufikia alipo sasa.
Nyota njema huonekana asubuhi, na kwa Dudu Baya, mapenzi yake kwa muziki hayakuanza juzi wala jana. Alipokuwa anasoma, alitumia muda wa ziada kuimba katika vikundi kanisani na inasadikika kuwa hilo ni moja ya motisha wake kuingia kwenye fani muda ulipowadia.
Mambo yalianza kushika kasi pale alipojisogeza Morogoro katika kupata Elimu zaidi, na ndipo alipotambulishwa rasmi katika muziki kufuatia mapenzi yake kwa kazi za Marehemu Tupac, Mr II na Afande Sele. Katika siku za awali alijulikana zaidi kama Double G ama “Godfrey Gangster” na alifanya maonesho kadhaa kwa mualiko wa wasanii nguli nchini, na hao ndio waliomsaidia kupata kujiamini zaidi kuwa anaweza pata mafanikio.
Nyimbo yake ya “Mwanangu Huna Nidhamu” aliyotengenezea MJ Records ni moja ya nyimbo zilizompa umaarufu wa ghafla Dudu Baya, ikifuatiwa na kazi nyingine kama “Siku Ya Kufa Kwangu”, “Dege la Jeshi”,”Amri 10 za Mungu”, “Tupa Mawe” na “Kunguru Hafugiki”. Wimbo wa “Nakupenda Tu” ni mmoja kati ya Nyimbo zilizopata kupendwa sana sio tu Tanzania bali Afrika Mashariki, na muda si muda Dudu Baya alijikuta akifanya kazi na watayarishaji muziki toka Kenya na Uganda na kupata ufuasi mkubwa sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Hivi sasa ana mapishi anayoyafanya chini kwa chini, na alipokutana na Crew ya Mkasi TV, alikua na mengi ya kusema! Tumia muda wako na umsikilize akitueleza mwenyewe hapa hapa!
Enjoy!
L•O•V•E

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support