Wednesday, March 20, 2013

NANCY SUMARI AZINDUA KITABU CHAKE KIPYA KIITWACHO "NYOTA YAKO"

 
Miss World Africa mwaka 2005 na Miss Tanzania mwaka huo huo, Nancy Sumari (pichani) jana alizindua Kitabu chake kiitwacho ‘Nyota Yako’, ambacho ni Kitabu cha simulizi inayohadithia mafanikio na uwezo wa wanawake tofauti wa Kitanzania wanaoonyesha jitihada na upekee unaolenga kumhamasisha mtoto wa kike kwenye jamii kutaka kuota ndoto kubwa na kudhubutu
kuyafanikisha yale ayawazayo.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitabu hiki cha ‘Nyota Yako’ alikua Profesa Esther Mwaikambo, ambaye alikua mwanamke wa Tanzania kuwa daktari, muanzilishi wa MEWATA na rais wa chama cha wanasayanzi Tanzania. Prof Mwaikambo pia ni daktari wa watoto katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es salaam, na ni moja kati ya hadithi ya wanawake ambao hadithi zao zimesimuliwa kwenye kitabu.


Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Kitabu hicho imefanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na baadhi ya wageni maalum waliofanikiwa kufika katika hafla hiyo ya uzinduzi ambao ni pamoja na Faraja Kotta Nyalandu, Fina Mango, Jacqueline Ntuyabaliwe, Sophia Byanaku, Jokate Mwegelo, Shamim Mwasha, Khadija Mwanamboka, na wadau wa habari pamoja na marafiki
Nancy Sumari (kushoto) akiwa na Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Profesa Esther Mwaikambo wakionyesha kitabu hicho mara baada yakukizindua. Kati kati ni Mtoto wa Nancy Sumari.
Nancy Sumari akiwa na Jacqueline Ntuyebaliwe (shoto) pamoja na Faraja Kotta wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Nancy Sumari akisaini moja ya kitabu kabla ya kumpatia Mwanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamepewa vitabu hivyo.


Nancy Sumari na Jokate Mwegelo. [habari, picha zote na michuzi]

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support