Wednesday, April 17, 2013

MADEE KUTOA VERSION MBILI ZA "POMBE YANGU"

Mwezi huu wa nne ndio mwezi ambao madee amepata mafanikio kwa mara nyingine tena, baada ya kuachia ngoma inayofanya vizuri sana kwenye chati mbali
mbali na kwenye maskio na midomo ya watu wengi, hata kufikia kuingia katika nafasi ya kwanza kwenye best chat show bongo "top 20" ya Clouds Fm.
Lakini pia ni mwezi ambao amezaliwa yeye, na kufikisha miaka yake kadhaa siku ya tarehe 23, na tarehe 21 anatarajia kufanya uzinduzi wa video ya wimbo wake "pombe yangu" ndani ya maisha club,Madee anatarajia kuachia video mbili za wimbo huo, moja ikiwa ni ya kiasili na nyingine ya kimjini mjini.
Licha ya kuachia video hizo, Madee pia atatoa dvd kwa mashabiki kwenda kuzitazama ka muda wao kutokana na kuelewa matatizo yanayotokana na kuhamia kwenye digitali.
kwenye show ya uzinduzi huo, atakuwepo pia , Bibi cheka, Diamond pamoja na Tunda man.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support