Wednesday, May 29, 2013

NGWEA KUZIKWA MOROGORO

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  na Baba yake mdogo kupitia East Africa Radio leo Asubuhi,

mazishi ya rapper Albert Mangwea aliyefariki Jana katika hospitali ya St.Helen Jijini Johannesburg,Africa Kusini yanaweza kufanyika mjini Morogoro.
"Tumekubalia kwamba tumelazimika kuzika Morogoro kwasababu kaka yetu ambaye ni baba wa marehemu tumemzika pale morogoro na familia yote ya marehemu ipo pale Morogoro.
Lakini hapa Dar es salaam tutafanya mapokezi na msiba utakuwa hapo kwa kaka yangu maeneo ya  Mbezi.
Kwa hiyo tutakuwa kwa kaka yangu anaitwa David Mangwea" Amesema.
Mpaka sasa bado haijajulika mwili wa marehemu Mangwea utakuja lini nchini.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support