Wednesday, May 29, 2013

WASANII WAAHIRISHA SHOW ZAO KWA HESHIMA YA NGWEA

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamechukua hatua na kuahirisha shughuli za
burudani zilizokuwa zifanyike weekend hii,Kati ya show zilizokuwa zifanyike weekend hii ni pamoja na show ya "The Finest" ya Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ambaye ametangaza kuiahirisha na kuisogeza hadi June 14.
Show nyingine kubwa iliyoahirishwa ni ya "Miaka 13 ya Lady Jaydee" iliyokuwa ifanyike May 31.
 Show nyingine iliyoahirishwa ni show ya kikosi cha mizinga wakiongozwa na kalapina ambayo nayo haitafanyika kama ilivyokuwa imetangazwa.
Mwana Hip Hop Izzo B alitarajia kufanya show weekend hii mkoani Mbeya pia ameahirisha show hiyo kuupisha msiba huu.
Khalid Mohamed a.k.a T.I.D kupitia ukurasa wake wa facebook alieleza maamuzi yake ya kuahirisha show aliyotarajia kufanya Maisha Club jana usiku pamoja na show ya Bukoba.
Wasanii wengine ni pamoja na Ben Pol ambaye ameahirisha kutoa video ya nyimbo yake mpya ya "Jikubali" aliyotarajia kuitoa June 1.
Msanii mwingine ni Joh Makini pia nae ameahirisha kutoa ngoma yake mpya aliyotarajia kuitoa May 30 mpaka atakapotaja tarehe mpya.pia ameahirisha kufanya show aliyotegemea kufanya Club 77.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support