Monday, May 27, 2013

PICHA ZA UZINDUZI WA MARCO CHALI FOUNDATION NA EPIC OPEN MIC ILIVYOFANA MWEMBE YANGA TEMEKE

Diamond na Ney wa Mitego

Godzilla

Mabeste

Madee

Prod. wa Mj Records ,Marco Chali akitoa maelezo kuhusu Foundation yake na Epic Open Mic

Rama Dee na Mapacha

Mshindi wa EBSS Walter Chilambo akiimba kwenye tamasha hilo.
Katika kuelekea msimu wa sita wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, kampuni ya simu za mikononi ya Zantel jana imezindua Epiq Open Mic ikiwa ni nafasi nyingine kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha vipaji vyao kabla usaili wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.

Epiq Open Mic inatarajiwa kuwapa nafasi vijana kujifunza misingi ya muziki kutoka kwa mmoja wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini, Marco Chali.

Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.

Tamasha hilo la Epiq Open Mic, ambalo ni la bure lilizinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke tarehe 26 ya mwezi huu ikisindikizwa na wakali kibao wa Bongo flavor kama Diamond Platnumz, Madee, Godzila, Ney wa Mitego, Mabeste na Mrap.


Baada ya uzinduzi wa tamasha la Epiq Open Mic Mwembe Yanga tamasha hilo litaendelea kila jumamosi kwenye makao makuu ya Zantel likiwapa nafasi vijana kujisajili na kurekod sauti zao.

Vijana watakaorekodi sauti zao watapigiwa simu na timu ya watayarishaji wa muziki chini ya Marco Chali pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri wa namna ya kuboresha muziki wao zaidi.

‘Zantel imejipanga kutumia fursa hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan.

Epiq Open Mic pia inatarajia kuwapa fursa ya kurekodi baadhi ya vijana watakaokua na vipaji.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support